Women WC 2018 Q: The Tanzanite wadai Nigeria walichezesha vijeba.

Timu ya Soka ya Taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 'The Tanzanite' wamepoteza mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Nigeria 'Falconers'.

Tanzania wamepoteza kwa mabao 3-0 katika mchezo ambao umefanyika Jana kwenye uwanja wa Samuel Ogbemedia Mjini Benin katika Jimbo la Edo, nchini Nigeria.

Mabao ya wenyeji yamefungwa na Rasheedat Ajibade Aliyefunga mabao mawili katika dakika ya 52 na 57 na Lilian Tule aliyefunga dakika ya 22.

Uchovu umechangia. 

Kocha msaidizi wa The Tanzanite Edna Lema ambaye hakuambatana na kikosi hicho amesema sababu kubwa ya kupoteza mchezo huo inawezakana kuwa ni uchovu wa safari kwani walifika siku moja kabla ya mchezo huo.

-Wale timu yao ni wakubwa mimi si nawajua ndo hao hao wanabadilika kucheza senior na kwa watoto pia, Sasa ukiwa na wachezaji wakubwa 10 na wadogo 15 sasa hyo si timu nzima?" Alisema Edna akitaja sababu nyingine ya kupoteza mchezo huo.

Timu hizo zitarudiana tena Septemba 29 Jijini Dar es Salaam, ikiwa Tanzania watahitaji ushindi wa zaidi ya mabao manne ili Kufuzu na kucheza na mshindi kati Morocco au Senegal katika hatua inayofuata.

The Tanzanite wanatafuta nafasi ya kufuzu kwenye fainali za Kombe la dunia kwa mara ya kwanza, fainali ambazo zitafanyika mwakani nchini Ufaransa.